MUME wa Khloe Kardashia, Lamar Odom, ambaye alikuwa nyota wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, ametoka hospitali baada ya kulazwa kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ligi ya NBA, alikimbizwa hospitalini mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu kwa kuzidiwa na matumizi ya dawa za kulevya.
Odom alilazwa katika Hospitali ya Cedars-Sinai iliyopo Los Angeles, lakini juzi aliruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na hali yake kuwa nzuri.
Khloe amedai kwamba amekuwa na furaha kubwa kuona mpenzi wake akiwa katika hali nzuri.
“Ni kitendo cha kumshukuru Mungu, amekaa sana hospitali lakini kwa sasa amepata nafuu na tuko naye nyumbani,” alisema Khloe.