24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

Annalu kuvuruga penzi la Tyga na Kylie

AnnaluNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO wa nchini Brazil, Annalu Cardoso, analitafuta penzi la mkali wa hip hop nchini Marekani, Tyga bila kujali uhusiano na Kylie Janner.

Mrembo huyo alifunga safari kutoka Brazil na kuja Marekani kwa ajili ya kukutana na Tyga, ambapo awali alionesha lengo la kutaka kujifunza muziki wa hip hop kutoka kwa Tyga, lakini kumbe alikuwa na lengo la kutoka kimapenzi na msanii huyo.

Baada ya kukutana na Tyga alionesha wazi kuwa hana lengo la muziki huku akionesha anataka mapenzi, lakini Tyga alimchomolea mrembo huyo na kumwambia kwamba ana mpenzi ambaye kila mmoja anamjua, Kylie.

“Anaonesha kuwa ananipenda, lakini sina mpango kwa kuwa nina mpenzi ambaye ananipenda na ninampenda, ila kama kazi ya muziki niko tayari,” alisema Tyga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,082FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles