27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

MUHIMBILI YAZINDUA KAMATI KUSIMAMIA MAADILI

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imezindua kamati mbili ambazo ni Kamati ya Uratibu na Kamati ya Kudhibiti Uadilifu, zitakazosimamia suala la maadili hospitalini hapo.

Kamati hizo zimezinduliwa leo Alhamisi Machi 15, na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Muhimbili, Hellen Mkondya ambaye pamoja na mambo mengine amewataka wajumbe walioteuliwa kuongoza katika kamati hizo kuhakikisha wanasimamia maadili ya kitaaluma.

“Hakikisheni mnakuwa mfano wa kuigwa katika kudhibiti na kupambana na rushwa, simamieni kuhakikisha haki ya mteja inalindwa, simamieni utawala bora kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma,” amesema.

Amesema kamati hizo zimeundwa wakati mwafaka na kwamba Muhimbili wanaunga mkono juhudi za serikali katika mapambano hayo, kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa na Mpango wa Utekelezaji awamu ya tatu mwaka 2017/24.

“Utawala bora ni pamoja na kusimamia Taasisi hasa kudhibiti na kupambana na rushwa kulingana na miongozo na sera zilizowekwa.

Awali, akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kamati hiyo ni majukumu mazito kwani ndiyo itakayosimamia utendaji wa hospitali kuhakikisha unafuata miongozo ya serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles