22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

MWILI WA MFANYABIASHARA ‘SUPER SAMI’ WAOKOTWA MTONI

Na Mwandishi Wetu

Mwili wa Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu Super Sami umepatikana Mto Rubana, Wilaya ya Bunda mkoani Mara ukiwa umefungwa katika viroba na kuharibika vibaya.

Kaka wa mfanyabishara huyo, Amini Sambo amekiri kuutambua mwili wa ndugu yake na kubainisha kuwa umekutwa ukiwa katika hali mbaya kutokana na kuanza kuharibika na sasa wanachosubiri ni uchunguzi wa polisi.

“Tumeutambua ni mwili wa ndugu yetu kweli, umepatikana Mto Rubana lakini kwa sasa tunasubiri uchunguzi wa kina wa mwili huo, nadhani baada ya hapo tunaweza kuongea lolote,” ameeleza Sambo.

Mfanyabishara huyo anadaiwa kutoweka Februari 27, mwaka huu nyumbani kwake eneo la Mwananchi-Buzuruga, Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza na Machi 9 gari lake aina ya Nissan Patrol lenye namba T 323 BSF lilipatikana Serengeti mkoani Mara, likiwa limeteketea kwa moto kando kukiwa na panga na kiberiti huku akidaiwa kukutwa amefariki lakini mwili haukuonekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles