28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MUHIMBILI YATOA NENO VICHANGA VILIVYOFARIKI

Na MWANDISHI WETU– DAR ES SALAAM


UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umeeleza kuhusu  vifo vya watoto njiti vilivyodaiwa kutokea hospitalini hapo mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru, alisema ingawa ni kweli kuna vifo vya watoto vilivyotokea hospitalini hapo  siyo kwa idadi kubwa kama ilivyodaiwa na vyombo vya habari.

“Muhimbili tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu habari iliyochapishwa juzi yenye kichwa cha habari ‘mshtuko vifo vya watoto Muhimbili’.

“Habari hiyo ilieleza kwamba  idadi kubwa ya watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda  wanahofiwa kufariki dunia katika hospitali yetu baada ya kukosa hewa ya oksijeni.

“Si kweli kwamba  Januari 13, mwaka huu, idadi kubwa ya watoto walifariki dunia  kwa sababu  kumbukumbu za hospitali zinaonyesha watoto watatu walipoteza maisha.

“Pia, umeme unapokatika, hauathiri mfumo wa oksijeni kwa vile  watoto huendelea kupata huduma hiyo kama inavyotakiwa.

“Lakini, katika jengo lile walimokuwa wale watoto, kuna ‘standby generator’ ambayo ikitokea umeme umekatika, lenyewe huendelea kuwasha umeme mara moja na kazi zinaendelea kama kawaida.

“Kwa wastani, watoto wanaopoteza maisha kwa siku hapa hospitalini kwetu ni wawili hadi wanne kati ya 110 hadi 128 wanaozaliwa kwa siku,” alisema Profesa Museru.

Taarifa ya hospitali hiyo iliyoandikwa katika daftari la usajili, ilieleza kwamba  idadi ya watoto  waliozaliwa kabla ya muda na kufariki dunia kuanzia Januari 10 hadi 15, mwaka huu ni watoto 13.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Januari 10, mwaka huu, walilazwa watoto 125 na wawili walifariki dunia wakati Januari 11, mwaka huu, walilazwa watoto 122 na waliokufa walikuwa wawili.

“Januari 12, mwaka huu, waliolazwa walikuwa watoto 103  na waliofariki dunia walikuwa ni wawili, Januari 13, mwaka huu, waliolazwa walikuwa 112 na watatu walikufa.

“Januari 14, mwaka huu, watoto waliolazwa ni 113 huku walifariki dunia ni watatu na Januari 15, mwaka huu, waliolazwa ni 109 na mmoja alikufa,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Museru, sababu zinazochangia kufariki dunia kwa watoto ni kuzaliwa kabla ya muda na kupungukiwa hewa wakati wa kuzaliwa.

Hata hivyo, alisema mbali na kuboresha  huduma na miundombinu katika wodi za watoto wanaozaliwa kabla ya muda na watoto kupatiwa dawa za kukomaza mapafu bila kujali uwezo mdogo wa  fedha wa mama aliyejifungua, kumesaidia watoto wengi wa kundi hilo kutoka salama kwa zaidi ya asilimia 90.

Pia, alisema gharama za dawa kwa ajili ya watoto hao ni kati ya Sh 580,000 hadi Sh 1,000,000 kwa mtoto mmoja kutegemea uzito wa mtoto husika.

“Pamoja na hayo kuwapo madaktari na wauguzi waliobobea katika maeneo ya kutolea huduma  kumesaidia kuleta mabadiliko makubwa ya afya bora kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda,” alisema.

Pamoja na ufafanuzi huo, MTANZANIA lilitembelea wodi namba 36 iliyopo jengo la wazazi na kushuhudia jinsi watoto wanavyoendelea kupatiwa huduma bora.

Muuguzi ambaye pia ni mtaalamu wa mashine ya oksijeni, Salum Seif, alieleza jinsi   mashine hizo zinavyofanya kazi.

Alisema  mashine hizo hazihusiani  kwa namna yoyote na umeme unaosambazwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

“Hizo mashine haziunganishwi na umeme bali zinajitegemea na kuna kifaa ambacho kinasaidia kujua kiwango cha oksijeni kinachohitajika.

“Kifaa hicho kinaposoma namba 48 au 49, hicho ni kiwango sahihi lakini kikizidi namba 50 na kuendelea hapo tunajua hewa imepungua.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles