31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Muheza kupata maji ya uhakika 2021

Na Amina Omari, Tanga

Serikali imewahakikishia wamamchi wilayani Muheza mkoani Tanga kuwa ifikapo Februari, 2021 watakuwa na wamepata huduma ya uhakika ya maji safi na salama.

Hatua hiyo inakuja baada ya utekezaji wa awamu ya mwisho ya ukamilikaji wa mradi wa maji wa Pongwe – Muheza unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira jijini Tanga (Tanga-UWASA) kwa gharama ya Sh bilioni 6.1.

Akizungumza leo Jumapili, Desemba 20, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Naibu Waziri wa maji, Mhandisi Marryprisca Mahundi amewataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani na serikali yao kwani inajitahidi kumaliza kero hiyo.

“Tunatarajia kumlipa mkandarasi malipo yake ya mwisho mapema mwezi January hivyo matarajio yetu mpaka ifikapo mwezi wa pili wananchi wataachana na kupata maji kwa mgao” amesema Mahundi.

Aidha, amepongeza jitihada za Tanga-UWASA za kulinda na kutunza chanzo cha maji cha bwawa la Mabayani hali ambayo imesaidia kuweza kuhudumia wilaya mbili za Tanga na Muheza bila ya chanzo hicho kukauka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles