28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Maswa wamlilia Dk. Ng’wandu

Na Samwel Mwanga,Maswa

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameonyesha kushikitishwa na taarifa za kifo cha, Dk. Pius Yasebasi Ng’wandu

Dk. Ng’wandu aliyewahi kuwa Mbunge wa Maswa amefariki dunia katika Hospitali ya mkoa wa Simiyu iliyoko mjini Bariadi alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Wakizungumza kwa masikitiko nyumbani kwake maeneo ya Uzunguni mjini Maswa wamesema kuwa wilaya hiyo imempoteza kiongozi ambaye alikuwa mshauri mzuri.

Wamesema kuwa marehemu atakumbukwa na wananchi wa wilaya hiyo wakati akiwa Mbunge wa jimbo hilo aliweza kuhakikisha wanapata mradi mkubwa wa maji safi na salama.

“Haya maji ambayo tunayatumia hapa mjini Maswa na vijiji vipatavyo 11 yalipatikana wakati wa uongozi wake kwa kweli ameacha alama kubwa sana,”amesema Omari Iddy.

Wamesema kuwa yale mambo ya msingi ambayo ameyaacha ni vizuri yakaendelezwa ikiwa ni sehemu ya kuenzi mambo aliyoyafanya wakati wa uhai hasa kwa maendeleo ya wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge mbali na kusikitishwa na kifo hicho cha ghafla cha Dk. Ng’wandu amewomba wakazi wa wilaya hiyo kuwa watulivu wakati taratibu za mazishi zikifanyika na wakapewa utaratibu mzima na mahali na siku ambayo mazishi hayo yatafanyika.

Dk. Ng’wandu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali enzi za uhai wake kwani amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japani,Waziri wa Maji na Waziri wa Sayansi na Teknolojia na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles