30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mavunde amwaga vifaa ufunguzi ligi ya Mkoa

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde amefungua mashindano ya mpira wa miguu ya Ligi ya Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya Shell Chamwino huku akiwataka vijana kutumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao na kujitangaza.

Mavunde amefanya uzinduzi huo jana Jumamosi Desemba 19, jijini humo huku akiwahimiza vijana kuwa na malengo ya ya kucheza ligi daraja la kwanza na ligi kuu.

“Tumieni mashindano haya kama sehemu ya kujiweka sokoni na kuvutia vilabu vikubwa kuhitaji huduma yenu. Michezo ni ajira, hivyo wekezeni nguvu nyingi na maarifa katika kukuza vipaji vyenu ili viwafae katika maisha yenu na kuwa sehemu ya mabadiliko ya maisha yenu,” amesema Mavunde

Aidha, Ufunguzi huo ulihusisha mechi ya awali kati ya timu za Ntyuka na Zejele-Bahi.

Wakati huo huo Mbunge Mavunde ametumia fursa hiyo kugawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh 6,000,000 kwa timu zote 15 za Dodoma Jiji zinazoshiriki katika mashindano hayo ya Ligi ya Mkoa na kuwataka kuhakikisha kwamba ubingwa wa Ligi ya Mkoa unabaki Dodoma Jiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles