28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Deep Jahi, DeeClef, Buffalo Souljah watikisa na ‘Guide My Path’

Na Christopher Msekena

Licha ya janga la corona kuathiri mataifa mengi ulimwenguni wasanii nyota kutoka Jamaica, Deep Jahi na DeeClef wakishirikiana na mkali wa Dancehall Afrika Kusini, Buffalo Souljah wanatikisa na wimbo wao mpya wa Inspiration, Guide My Path.

Ngoma hiyo iliyotoka hivi karibuni katika mitandao mbalimbali ya kuuza na kusikiliza muziki, imetengenezwa na Jerome Elvie chini ya lebo ya Natural Bond Entertainment ambapo alifurahia kufanya kazi na vipaji hivyo.

“Nimefanya kazi na wasanii hawa wenye talanta kwenye moja ya project yangu ya hivi karibuni inayoitwa Gold Leaf Rhythm naamini mashabiki wengi wamependa ushirikiano huu, DeeClef alikuwa wa kwanza kati ya wale watatu kusikia biti kulingana na kile kinachoendelea ulimwenguni leo, kila msanii aliamua tu kuonyesha uwezo wake kwenye mdundo kuhusu corona,” anasema Elvie.

Akizungumza na Mtanzaniadigital hivi karibuni, DeeClef ambaye ni mzaliwa wa Jamaica anayeishi New York, Marekani alisema: “Katika nyakati kama hizi ambapo ulimwengu unapitia janga la corona, nilipata hisia za kufanya jambo kwaajili ya mashabiki nikiwapa hamasa ya kuendelea kumwomba Mungu na nimefurahi kuwa sehemu ya mradi huu.”

Naye Buffalo Souljah anasema: “Hii ni ngoma kubwa sana na ina ujumbe mzuri ambao ni jambo ambalo Waafrika wengi wanaweza kujihusisha nalo. Kufikia sasa mapokezi ni makubwa kutoka kwa mashabiki hasa ladha ya Reggae na Dancehall niliyoiweka na video ya Guide My Path itatoka hivi karibuni hiyo itatupeleka mbali zaidi na kufikisha ujumbe kwa jamii.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles