29.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 30, 2024

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MTUWASA KUKUSANYA MADENI KIELEKTRONIKI

Na Florence Sanawa, Mtwara

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara Mjini (MTUWASA), imeanzisha utaratibu mpya ya kulipia madeni yake kwa njia ya elektroniki kupitia mtandao wa simu za mkononi (NMB Mobile) ili kurahisisha ukusanyaji madeni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza na na waandishi wa habari Ofisa Biashara wa MTUWASA, Judith Namwereni amesema ukusanyaji huo kwa njia ya kielektroniki utaongeza hamasa kwa watu wengi kutumia huduma hiyo.

“Wateja wetu ni wengi ndiyo maana tumefanya mazungumzo na benki hii ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato hata ukiangalia watumiaji wa benki kwa sasa ni wengi kwa hiyo ili kuwapunguzia safari ya kuja kulipa ofisini sasa wanaweza kulipia kupitia simu zao za kiganjani huduma hii inaenda na wakati na iko kidigitali zaidi.

“Wako watu wanatumia maji hadi miezi sita bila kulipa huenda ikawa umbali sasa tumerahisisha ili kupunguza mlundikano wa madeni uliokuwepo waone umuhimu wa kulipia huduma ya maji wanayopata kupitia mamlaka hii,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Kanda ya Kusini, Haji Msingwa amesema kutokana na idadi kubwa ya Watanzania kutumia simu za mkononi itaongeza hamasa kwa wateja wa mamlaka hiyo kulipia maji kupitia NMB mobile.

“Tumejipanga kuhakikisha kila kijiji na kata anakuwapo Wakala wa NMB Mobile ili kurahisisha watumiaji wa huduma hiyo kufanya malipo na mihamala mbalimbali ili twende kidijitali zaidi na kuacha njia za zamani ambazo zimekuwa zikipoteza muda kwa wateja wetu,” amesema Msingwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles