27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: SUKARI INAYOZALISHWA NCHINI HAITOSHELEZI

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais John Magufuli, amesema sukari inayozalishwa nchini haitoshelezi kutokana na uwekezaji mdogo uliowekwa katika kilimo cha miwa.

Amesema kutokana na hali hiyo wafanyabiashara ndiyo  wengi wanalazimika kuagiza sukari nje ya nchi.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi katika Mkutano wa Mwaka wa 11, wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Machi 19.

“Mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 590 lakini zinazozalishwa ni tani 335 hali inayolazimu kuagiza sukari kutoka nje ya nchi wakati kuna viwanda vinazalisha sukari hapa nchini hii ni kutokana na uwekezaji mdogo uliowekwa katika kilimo cha miwa.

“Kwanini tuendelee kuagiza sukari nje tumeshindwa kuzalisha  hizo tani hapa nchini, na suala la sukari limewagharimu hata mawaziri wengi tangu enzi za Nyerere,” amesema.

Aidha, amesema wafanyabiashara wengi hawafuati sheria za biashara ikiwamo kulipa kodi kwa wakati na ikifika wakati wa bunge wanahamia Dodoma ili kuwarubuni wabunge kutopitisha sheria zitakazowabana na tabia kama hizi ndiyo zinasababisha kuwepo na viwanda hewa kama Maisha Bottlers.

Pamoja na mambo mengine, amewataka wafanyabiashara nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwamo kilimo na ufugaji ili kupunguza uagizwaji wa bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa ndani ya nchi na kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Aidha, Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendeleza amani iliyopo kwa kuwa ndiyo ilikuwa moja ya chachu ya uwekezaji wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda na wasirubuniwe na watu wachache wanaowashawishi kufanya vitu vinavoashiria kuvuruga amani ikiwamo maandamano badala yake watumie muda huo kufanya kazi ili kukuza uchumi wa nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles