27.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi wa afya afikishwa mahakamani kwa tuhuma ya rushwa

Abdallah Amiri, Igunga, Tabora

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemfikisha Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga, mtumishi wa idara ya afya anayeishi Mtaa wa Masanga kata ya Igunga anayefanya kazi katika hospitali ya wilaya ya Igunga Wallace Joseph Kazili miaka 52 kwa kosa la kuomba rushwa ya sh. 200,000/= toka kwa mgonjwa.

Awali Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wilaya ya Igunga, Mazengo Joseph aliiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Lydia Ilunda kuwa mshtakiwa Wallace Kazili alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa No. 11, 2007.

Alidai Oktoba 30,mwaka jana, mshtakiwa Kazili akiwa Hospitali ya Wilaya ya Igunga kama nesi aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa Kasembe Nangale mkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ili ampatie dawa ya TB  kutokana na ndugu yake Bugumba Lisawi  kulazwa hospitalini hapo.

Alisema katika tarehe hiyo mwezi huo, Kazili alipokea Sh 50,000 kwa njia ya simu kama malipo ya awali ya Sh 200,000 alizoomba.

Alisema Novemba  mosi, mwaka huo huo,mshtakiwa  alipokea Sh 50,000 tena kama malipo mengine ya awali na kufanya   jumla ya Sh 100,000 alizopokea kati ya Sh 200,000.

Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 10, mwaka huu,itakapoanza kusikilizwa na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana ya Sh 300,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles