26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

TDA chatembelea kliniki 14 kutoa elimu ugonjwa wa kisukari

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

CHAMA cha  Ugonjwa wa Kisukari (TDA), kimefanya ziara katika kliniki 14 za kisukari nchini  na kutoa  elimu kwa watoto wenye ugonjwa wa kisukari aina ya kwanza, lengo likiwa kuwawezesha kujitambua na kuishi na ugonjwa huo, sanjari na kuelimisha wazazi na watoa huduma namna bora ya kuwahudumia watoto hao.

Mratibu wa TDA, Happy Nchimbi alisema katika ziara hiyo, watoto wenye ugonjwa wa kisukari waliopatiwa mafunzo kupitia kambi za kisukari mikoa ya Dodoma na Pwani Septemba mwaka huu, walitumika kama walimu kuelimisha wenzao kuhusu ugonjwa huo ambapo pia wazazi wa wenye matatizo hayo walielimisha wazazi wenzao, huku madaktari bingwa wakitumika kutoa elimu hiyo kwa watoa huduma na wauguzi.

Alisema kliniki hizo zilizotembelewa zinahudumiwa na chama hicho kwa dawa na kinga, ambapo watoto walielimishwa pia namna ya kujitunza, huku wazazi wakielimishwa namna ya kuishi na watoto wenye kisukari na kutokata tamaa kutokana na watoto wao kuugua.

“ Bado tupo katika mwezi ambao kuna maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza, chama hakitachoka kutoa elimu kuhusu kisukari aina ya kwanza, tukitambua ni tatizo kubwa kwani linawapata zaidi watoto. Wenye watoto walio na tatizo hilo wengi hukata tamaa, lakini hawapaswi kufanya hivyo, nasi tunawaelimusha ili kuwawezesha kuishi vizuri na kufikia malengo yao,  wauguzi na wazazi nao kutimiza wajibu wao kwa kuwasaidia watoto kwa huduma bora na kuwalea inavyostahili,” alisema.

Alisema  elimu  inalenga pia kuwawezesha kujikinga dhidi ya madhara ya ugonjwa wa kisukari aina ya kwanza akieleza  chama hicho kinawatumia wataalam wa lishe kusaidia kuelimisha watoto wenye ugonjwa huo namna nzuri ya ulaji.

“Chama kinatekeleza jukumu hili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ustawi wa jamii,Jinsia, Wazee na Watoto. Watoto zaidi ya 4,000 wanaugua kisukari aina ya kwanza nchini, lakini wapo pia wengi ambao pengine wana tatizo hilo na hawafahamu, muhimu ni kwenda kupima afya mara kwa mara hasa wanapoona dalili zisizo za kawaida kwa watoto,” alisema.

Katika hatua nyingine, alisema wamewazawadia vyeti wuguzi kutokana na  kutambua mchango wao katika kuwahudumia watoto wenye kisukari wakikumbuka kauli mbiu ya mwaka 2020 ya maadhimisho ya siku ya kisukari duniani isemayo; wauguzi na ugonjwa wa kisukari. Wao ndio huwa wa kwanza kuwapokea na kuwahudumia. Tumetoa kwa wauguzi wote wanahudumia kliniki za kisukari na tunawaomba wasichoke kwani watoto ni wetu sote,” alisema.

Alisema wanatamani kuona watoto  wanapata huduma na malezi stahiki ili wafikie ndoto zao na kwamba elimu inahitajika zaidi pia kwa walimu na jamii ili kutambua kuhusu ugonjwa huo na kusawaidia watoto wanaosumbuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles