25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi TFS Kiteto anusurika kifo

MOHAMED HAMAD

Mtumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kiteto, Bonaventure Mosha (54), amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la watu wa Kijiji cha Njoge Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati akitekeleza majukumu yake ya Kiserikali.

Mosha ambaye ni Afisa misitu msaidizi alijeruhiwa na kundi la watu hao wakati wakisafisha mipaka na watumishi wenzake katika hifadhi ya mlima Njoge inayomilikiwa na vijiji viwili, Dongo kilichopo Wilayani Kiteto na Njoge iliyopo Kongwa.

“Nilinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la watu waliokuwa na mapanga, marungu ambao walianza kwa kuniuliza kwanini nafanya kazi ya kusafisha mipaka katika maeneo hayo ambayo wanayatumia miaka mingi iliyopita kwa shughuli za kilimo na ufugaji”

Alisema alianza kushambuliwa kisha kuvunjwa mkono wa kushoto, kujeruhiwa kichwani, na sehemu mbalimbali na mwili wake na aliyekuja kumwokoa ni mtendaji wa Kijiji cha Njoge, Paulina Ndaiga aliyefika na pikipiki na kuamuru aondolewa kwa haraka katika eneo hilo.

“Niliripoti Kituo cha Polisi Dongo Kiteto, na kupata PF3, ambayo ilinisaidia kwenda kupata matibabu Kituo cha Afya Sunya na Baadaye hospitali ya Wilaya ya Kiteto, hakika walinisaidia kuokoa maisha yangu kwani nilikuwa na hali mbaya, na hasa shukrani za pekee ni kwa mtendaji kwani ningekufa” amesema.

Kwa upande Meneja misitu Wilaya Elias Sweti, alisema tukio hilo limelenga kudhofisha shughuli za usimamizi wa mazingira ambapo kuna jitihada mbalimbali na kuokoa maeneo yaliyovamiwa na kuharibiwa na wananchi kwa shughuli za kilimo na ufugaji

“Tuna changamoto kubwa katika shughuli hii kwani kazi tuzifanyazo zinalenga kuhifadhi lakini wananchi wanavamia kwaajili ya matumizi ya wakati hii huku wakifanya uharibifu mkubwa wa misiti na vyanzo vya maji.

Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Kiteto kufuatia tukio hilo na hali ya majeruhi huyo inaendelea vyema huku shughuli hiyo ya kusafisha mipaka ikiwa imesimama kufuatia tukio la kujeruhiwa mtumishi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles