Mtumishi awakumbuka wanawake

0
599

mtumishi 3Na Ruth Mnkeni

CHIPUKIZI anayefanya vema katika muziki wa Bongo Fleva, Dani Mtumishi, amewataka wasanii wenzake waimbe nyimbo za mafunzo kwa rika mbalimbali hasa umuhimu wa wanawake katika jamii.

Mtumishi alieleza hayo baada ya kuachia wimbo wake mpya aliouita ‘Hivi kwa nini’ ambao amemuelezea mwanamke katika nyanja mbalimbali zinazoleta tija katika kusaka maendeleo kwa ujumla.

Mtumishi alishawahi kutoka na wimbo wa ‘Usishiriki wivu’ ambao alimshirikisha msanii maarufu Bongo Fleva, Rich Mavoko.

“Baada ya kumshirikisha, Rich Mavoko, katika wimbo ule mwaka huu nimeamua kurudi mwenyewe katika wimbo wa peke yangu nikiamini utanifikisha mbali licha ya kushirikisha wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo.” alieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here