23.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 2, 2024

Contact us: [email protected]

Mtu mmoja afariki katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Rwanda

Kigali, Rwanda

Mtu mmoja amefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa mvutano kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa rais wa Rwanda, Paul Kagame, maafisa wanasema.

Kampeni za uchaguzi mkuu wa Julai mosi zilianza Jumamosi, huku Kagame akifanya mikutano miwili kaskazini mwa Rwanda mwishoni mwa juma.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili wilayani Rubavu, ambapo watu 37 walijeruhiwa, wanne kati yao wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya, taarifa ya wizara ya serikali za mitaa ilisema.

Iliomba msamaha kwa familia ya marehemu, na kuongeza kuwa timu ya matibabu kwenyeeneo la mkasa “ilifanya kila linalowezekana”.

Kagame anawania muhula wa nne. Amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu 1994, wakati kundi lake la waasi la wakati huo, Rwanda Patriotic Front, lilipotwaa mamlaka mwishoni mwa mauaji ya kimbari yaliyoelekezwa kwa watu wa kabila lake la Watutsi.

Alishinda uchaguzi uliopita wa urais mnamo 2017 kwa karibu 99% ya kura.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 66 amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kukandamiza upinzani – lakini ametetea vikali rekodi ya Rwanda kuhusu haki za binadamu, akisema nchi yake inaheshimu uhuru wa kisiasa.

Baada ya mkanyagano wa Jumapili, wizara ya serikali za mitaa iliwakumbusha: “Wale wanaoshiriki katika shughuli za kampeni… kufuata maagizo yaliyotolewa na wasimamizi ili kuhakikisha usalama na utulivu wa wale wanaoshiriki katika shughuli za kampeni,”.

Paul Kagame na chama chake cha RPF Inkotanyi hawajatoa maoni yao kuhusu kifo hicho.

Hata hivyo, Jumatatu asubuhi, RPF Inotanyi ilichapisha video kwenye Facebook ya Kagame akipanda jukwaani kwenye mkutano huo. Takriban watu 250,000 walihudhuria mkutano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles