30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtihani wa Pinda kuanza leo Dodoma

PINDANa Debora Sanja, Dodoma
VIKAO vya Bunge la Bajeti ya mwaka 2015/16 vinaanza leo Dodoma huku Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ya kwanza kuwasilisha bajeti yake.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, mkutano huo wa 20 Bunge unatarajiwa kuanza leo hadi Juni 27 mwaka huu ambako Bunge hilo litavunjwa na nchi kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Waziri Mkuu Pinda atawasilisha bajeti ya ofisi yake ambayo inahusisha wizara tatu ambazo ni Ofisi ya Bunge, Sera, Uratibu na Bunge, Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Uwekezaji na Uwezeshaji.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu inatarajiwa kujadiliwa kwa siku tano kuanzia Mei 12 hadi Mei 16 mwaka huu.
Tofauti na Ofisi ya Waziri Mkuu, wizara tatu zilizopo chini ya ofisi ya Rais zenyewe zitajadiliwa kwa siku moja tu ambayo ni Mei 18 mwaka huu.
Wizara hizo ni Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais Utawala Bora na Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu.
Baadhi ya wizara mbili zilizopangwa kujadiliwa kwa siku moja ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambazo zitajadiliwa Mei 22 mwaka huu.
Nyingine ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Wizara ya Kazi na Ajira zikazojadiliwa Mei 25 mwaka huu huku Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia zikijadiliwa Mei 26 mwaka huu.
Bajeti Kuu ya Serikali inatarajiwa kusomwa Juni 11 mwaka huu, ikitanguliwa na kusomwa kwa taarifa ya hali ya uchumi.
Mjadala kuhusu wa bajeti unatarajiwa kuanza Juni 24 ambao kwa mujibu wa ratiba hiyo utakuwa wa siku saba.
Muswada wa Sheria ya Fedha unatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa Juni 25 na 26 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles