27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waliokufa kwa mafuriko Dar wafikia 12

KOVAAsifiwe George na Mgeni Shabani (EWTC)Dar es Salaam
IDADI ya watu waliofariki dunia kutokana na athari za mvua na mafuriko Dar es Salaam imeongezeka kutoka wanane na kufikia 12.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa kati ya watu hao mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35-38, mwili wake ulipoolewa baada ya kuzama kwenye tope katika mto Msimbazi, Magomeni.
Alisema mwili huo wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.
Kamanda aliyataja majina ya watu wengine waliofariki dunia kuwa ni Valerians Eradius (13) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kigogo ambaye alikufa Mei 10 mwaka huu baada ya kuangukiwa na ukuta.
Mwingine ni Gervas Shayo (28) mkazi wa Mbezi juu ambaye alikufa maji Mei 8 mwaka huu pamoja na mwanamke mmoja anayekadriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 ambaye jina lake halikufahamika ambaye alikutwa katika bonde la Mkwajuni akiwa amefariki dunia.
“Uzoefu unaonyesha kuwa jinsi maji yanavyoendelea kupungua kutokana na kupungua kwa mvua ndivyo madhara yanaonekana.
“Ninawaomba wananchi waendelee kutoa taarifa mapema wanapoona mwili wa mtu aliyekufa ili hatua zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na kuiondoa miili ya watu watakaokuwa wamekufa kutokana na athari za mvua inayoendelea kunyesha Dar es Salaam,” alisema Kova.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles