23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mtetemela sekondari yapatiwa vifaa vya milioni nne

MOHAMED HAMAD-KITETO

Shule ya Sekondari Mtetemela Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imepatiwa vifaa vya maabara ya sayansi vyenye thamani ya milioni nne kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi.

Vifaa hivyo vimetolewa na Wayoming kutoka Marekani, ambao wameamua kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli, kuboresha elimu wilayani humo.

Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Kiteto, Isaya Chamabala, akikabidhi vifaa hivyo uongozi wa shule hiyo, aliwataka wanafunzi kuvitunza ili viwe endelevu, huku akisisitiza waalimu kufundisha kwa bidii.

“Tumeletewa vifaa toka kwa Wayoming rafiki zetu wa Marekani ambavyo vitatumika kwa ajili ya maabara za masomo ya Physics, Biologia, na Chemestry, tunalenga kuongeza ufaulu wa wanafunzi,” amesema.

Amesema Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Kiteto, linaunga mkoni Jitihada za Serikali ya Rais Magufuli, katika Sekta ya elimu na kuwataka wanafunzi na waalimu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ambao ni kusoma na kufundisha kwa bidii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles