32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MTANZANIA MSHINDI WA KWANZA MASHINDANO YA QUR-AN

NA ASHA BANI-DAR ES SALAAM


MTANZANIA Mbwana Dadi kutoka mkoani Morogoro, ameibuka mshindi wa kwanza katika mashindo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur-an Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al- Hikma.

Dadi ambaye alipambana na washiriki wengine kutoka mataifa mengine ya Afrika, alikabidhiwa zawadi ya Sh milioni 15, kompyuta mpakato (laptop) na kiwanja eneo la Kigamboni baada ya kuhifadhi Juzuu 30.

Mashindano hayo yalishirikisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 10 ambapo Dadi aliibuka mshindi wa jumla.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Dar es Salaam jana katika mashindano hayo ya 19, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliwataka Waislamu nchini kutoyumbishwa katika kuhubiri amani kwani ni muhimu katika kuchochea maendeleo na uchumi wa viwanda.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka Waislamu kutokubali kudanganyika ili wasiingize nchi katika machafuko kwani uchumi wa viwanda na maendeleo ya nchi yanategemea amani na utulivu.

Majaliwa pia aliwataka waache kutumika vibaya na watu wenye masilahi binafsi kwani siku zote watu wa aina hiyo wanaondoa amani ya nchi iliyopo.

Alisema kuna tabia zimeanza kujitokeza katika siku za hivi karibuni kwamba taasisi na watu au viongozi wa taasisi zinazopigania amani kuambiwa zinajipendekeza kwa Serikali jambo ambalo si kweli.

“Tabia hizo hazina mashiko hasa katika nchi ambayo inataka kwenda katika uchumi wa viwanda, natumia jukwaa la mashindano haya kulisema hili kwani naona linaanza kuota mizizi na watu wenye fikra hizo wapuuzwe,” alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia mashindano hayo, alisema yamekuwa chachu na ni utambulisho wa nchi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono na watu wote.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles