25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MSIGWA: WANAOHAMA CHADEMA WASHAMBA WA KISIASA

 

Na Raymond minja, Iringa

 

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amesema wanaohama chama hicho na kukimbilia vyama vingine vya siasa ni washamba wa kisiasa walioshindwa kuheshimu dhamana kubwa waliyopewa na wananchi katika kuwatumikia. 

Kauli hiyo ya Msigwa inakuja siku moja baada ya Diwani wa Kata ya Gangilonga ambaye pia alikuwa ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Dady Igogo kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo udiwani jana.

Akizungumza na Mtanzania Digital kwa njia ya simu leo Alhamisi Februari 22, Msigwa amesema iko haja ya wananchi kuwapuuza watu hao kwani wameshindwa kuwa na utu na kuheshimu heshima kubwa waliyopewa na Watanzania kuwaongoza na badala yake wanakimbia majukumu.

“Hao watu ni wa kupuuzwa na wala hii si habari mpya kwetu tunajua nini wanafanya lakini niwaambie wana Iringa mimi na chama changu tuko imara hatuyumbishwi na hao wachache wanaoondoka na tutaendelea kuwatumikia kwa moyo mmoja,” amesema.

Aidha, katika sababu za kujiuzulu kwake katika nafasi hizo Igogo amesema ziko moyoni mwake na ameamua kuwa raia wa kawaida ambapo pia amewashukuru wananchi wa Gangilonga kwa kuwa naye katika kipindi kigumu alichopita katika siasa. 

Alipotakiwa atoe ufafanuzi wa sababu zilizopo ndani ya moyo wake na kipindi kigumu alichopita katika siasa alisema hana cha kufafanua japokuwa maamuzi hayo ni kwa faida ya maisha yake ambayo pia hakuyafafanua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles