31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MATUMIZI HOLELA UZAZI WA MPANGO SI SALAMA KIAFYA


NA JACKSON NYABUSANI  |   

KWA lugha rahisi, uzazi wa mpango ni njia ambazo wanandoa au watu waliopo katika uhusiano wa kimapenzi hutumia ili kuweza kupanga muda mwafaka wa kupata mtoto/watoto.

Sera ya uzazi wa mpango imekuwa ikipokewa kwa mtazamo tofauti katika jamii yetu. Kwa upande wa serikali, kumekuwapo jitihada za kuielimisha jamii kuhusu na jambo hilo.

Zipo njia mbalimbali za uzazi wa mpango, kwa ujumla wake tunaweza kuziweka katika makundi mawili ambayo ni kundi la njia za muda mfupi na lingine ni lile la njia za muda mrefu.

Njia za uzazi wa mpango za muda mfupi hujumuisha matumizi ya vidonge ambavyo mwanamke hutumia kwa kumeza kidonge kila siku, au kwa kuweka kidonge katika maumbile yake (ukeni) kabla ya kukutana na mwezi wake, au kwa kumeza kidonge ndani ya saa sabini na mbili baada ya kukutana na mwenzi wake.

Njia hii ya muda mfupi imekuwa ikitumika mara kwa mara na wanandoa na walio katika mapenzi kutokana na urahisi wake katika  kuitumia, kwa kuwa haihitaji ujuzi mkubwa na vifaa katika kuitumia.

Kwa upande wa njia za muda mrefu, kumekuwapo matumizi ya sindano pamoja na vipandikizi (Implants). Njia hii huhitaji utaalamu na baada ya mwanamke kuwekewa kipandikizi huweza kudumu kwa kipindi cha kuanzia miaka mitatu hadi mitano bila kupata ujauzito.

Pamoja na uwepo wa njia hizi mbili za muda mfupi na mrefu, pia kumekuwepo na njia ambazo zimekuwa zikitumika kupanga uzazi kama vile matumizi ya kondomu na kufuatisha kalenda ya mzunguko wa siku za hedhi kwa mwanamke.

Tumeweza kufahamishana njia zinazotumika katika uzazi wa mpango, miongoni mwa maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa ni pamoja na haya je, ni njia ipi sahihi ya uzazi wa mpango? Pia ni muda upi mwafaka unaofaa kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango?

Aina ya njia ya uzazi wa mpango pamoja na umri wa kuanza kutumia njia hizi ni mambo ya msingi katika kuhakikisha maudhi na madhara yanayoweza kusababishwa na njia hizi hayatokei. Mfano kuna baadhi ya watu ambao wamepatwa na maudhi madogo madogo yaliyosababishwa na matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama vile kuongezeka uzito, kupatwa na kichefuchefu pamoja na maudhi mengine yenye kufanana na hayo.

Siku zote elimu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango imekuwa ikitolewa kwa kukuelewesha wewe pamoja na mwezi wako kuchagua njia sahihi kulingana na hali yako ya kiafya.

Kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango bila ya kufuata ushauri wa kitaalamu  mfano matumizi ya vidonge imekuwa chanzo cha baadhi ya malalamiko na matatizo ya uzazi kwa baadhi ya watu.

Mfano mwingine ni kwa mtumiaji wa kipandikizi, huyu atahitajika kukitoa hicho kipandikizi baada ya miaka mitatu au mitano, lakini kwa umri alionao ambapo bado ni mwanafunzi wa darasa la saba ameanza kutumia njia hizi za vipandikizi, anaedelea nacho akiwa sekondari, chuo akiwa hadi anajikuta zaidi ya hiyo miaka mitatu au mitano yeye anaendelea na matumizi ya vipandikizi mfululizo.

Kwa kufanya hivi, mwili unajikuta  umetumia dawa husika kwa kipindi kirefu zaidi ya miaka ambayo imeandaliwa (mitatu/mitano) na athari zake zinaweza kuwa ni kuvurugika kwa tarehe za siku za hedhi na kushindwa kushika ujauzito katika muda au kipindi ambacho atahitaji.

Dawa za uzazi wa mpango pamoja na njia nyingine zote zinaweza kuwa sahihi na salama kulingana na ushauri utakaopewa na daktari kwa kuangalia taarifa zako za kiafya.

Kwa maoni na ushauri usisite kuwasiliana nami kupitia

0652 082765. Pia unaweza kutembelea tovuti www.tanzlife.co.tz

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles