29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MSIGWA APANDISHWA KIZIMBANI AKIDAIWA KUTISHIA KUUA

Na RAYMOND MINJA – IRINGA

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.

Diwani wa Viti Maalumu, Selestina Johanes na dereva wa mbunge huyo, Godi Mwaluka nao walipandishwa kizimbani kwa shitaka hilo.

Akisoma shtaka hilo jana, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Rehema Mayagilo alidai mbunge huyo na washtakiwa hao wawili wanadaiwa kumtusi na kutishia kumuua diwani huyo.

Hakimu Mayagilo alidai Msigwa na wenzake walitenda kosa hilo juzi   mchana katika viunga vya Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Mbali na kumfungulia kesi Msigwa, Kimata naye aligeuziwa kibao na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Dady Igogo na kisha kufunguliwa kesi ya kufanya vurugu kwenye ofisi za halimashauri hiyo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Msigwa na wenzake walipata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka huu itakapotajwa tena.

Wakizungumzia tukio hilo   baada ya kesi kuahirishwa Mchungaji Msigwa, alisema Kimata aliwakuta wametulia wakibadilishana mawazo nje ya ofisi ya mbunge huyo na mshtakiwa akalazimisha kusalimia.

Alisema   baada ya Msigwa kukataa kuitikia salamu yake, Kimata alianza kumtusi pamoja na diwani huyo   na dereva wake  jambo ambalo lilimkera mbunge huyo.

“Baada ya kukataa kupokea salamu yake, Kimata alianza kunitusi na kuniita dikteta, mara mimi kafupi, jambo ambalo sikulipenda.

“Lakini nilivumilia na kuwaita walinzi wamuamuru kuondoka eneo hilo lakini cha kushangaza alikimbilia polisi na kudai sisi ndiyo tumemtukana na kutishia kumwua jambo ambalo si kweli,”alisema Msigwa.

Naye Kimata ambaye alikuwa ni diwani wa Chadema na  kujiuzulu nafasi hiyo hivi karibuni, alidai   salamu si ugomvi na baada ya mbunge kukataa kupokea salamu aliamua kuondoka lakini mbunge huyo alimfuata na kuanza kumtusi na kutaka kumpiga akiwa pamoja na diwani na dereva wake.

“Nimesalimia hawajaitika nikaamua kuondoka lakini walinifuata na kuanza kunitukana huku wakitishia kunipiga nikaamua kwenda kushtaki polisi na kuwafungulia mashtaka,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles