24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mshindi Maisha Plus kusomea uandaaji wa filamu

Olive Kiarie
Olive Kiarie

BEATRICE KAIZA Na HADIA HAMIS- DAR ES SALAAM

MSHINDI wa Shindano la Maisha Plus msimu wa tano kutoka nchini Kenya, Olive  Kiarie, amesema atatumia fedha alizoshinda kujifunza taaluma ya uandaaji wa filamu.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili jana alipokuja kutoa shukrani kutokana na mchango mkubwa ulioonyeshwa na gazeti hilo kipindi chote cha mashindano hayo, Olive alisema mbali na kutumia fedha hizo kujifunza filamu, nyingine atazipeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima nchini Kenya.

Olive alisema anashukuru kuibuka na ushindi, hivyo ni vema akarudisha shukrani kwa wale waliofanikisha mafaniko yake.

“Nashukuru, kuwa mshindi ni kitu kikubwa, hivyo nimekuja kutoa cheti, kuonyesha jinsi gani nimethamini mchango ulioonyeshwa na gazeti hili.

“Nilipanga kutoa fungu la 10 la fedha nitakazoshinda kwa watoto yatima nyumbani kwetu, hilo lazima nilitimize,” alisema Olive.

Olive alieleza kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu wenye upendo, kupitia shindano hilo ameweza kujifunza mambo mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles