29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

MSAKO WA ‘VIROBA’ WAENDELEA DAR

Na ASHA BANI


MSAKO mkali wa kubaini wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa pombe kali zinazofungashwa katika paketi za plastiki, maarufu viroba unaendelea kutikisa Jiji la Dar es Salaam.

Jana timu inayoendesha msako huo ilikuwa katika maeneo ya Wazo Hill na kukamata shehena yenye katoni 7,000 zenye thamani ya Sh bilioni 2.

Mmiliki wa ghala lililopo Wazo Hill linalojulikana kama Lovekira Enterprises, ndiye huyo huyo aliyekutwa na shehena kubwa ya katoni 25,634 Kimara Temboni.

Mwanasheria wa Ofisi ya Mazingira, Heche Suguta, alisema wamekamata mzigo huo na kwamba wameufungia hadi hapo mmiliki atakapoutolea maelezo ya kutosha kutokana na kukiuka kanuni mbalimbali.

Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Nzila, alisema katika ghala la Lovekira Enterprises  wamekuta konyagi za milimita 100, katoni 14,393 za mililita 50.

Aina nyingine ya pombe iliyokamatwa katika ghala hilo ni Vradimil za milimita 50, zanzi 90, value 23 za mililita 50 na mililita 100 zikiwa 233 zenye  thamani ya Sh bilioni 3.18.

Suguta alisema zoezi hilo ni endelevu ili kuwabaini wanaoendelea na biashara hiyo licha ya Serikali kusitisha kwa mujibu wa kanuni na sheria mbalimbali za vileo.

Juzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba, alitangaza msako huo kuendelea huku kukiwa na jumla ya katoni 99,171 ya pombe kali kwenye vifungashio vya plastiki yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10.83. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles