28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

PROFESA LIPUMBA AGONGA MWAMBA KAMATI TENDAJI

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF), kimeshindwa kufanyika baada ya wajumbe wote wa kikao hicho kutoka Zanzibar kukisusia hivyo kufanya akidi ishindwe kutimia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi kuu ya chama hicho Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya, alisema wajumbe wote wa Tanzania bara na visiwani walipata taarifa za kikao ambapo wajumbe wa bara waliitikia lakini hakuna hata mmoja kutoka Zanzibar aliyeitikia wito.

Alisema kikao hicho kilitakiwa kuhudhuriwa na wajumbe 15 ambapo 7 ni kutoka Zanzibar na Tanzania bara 7 akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa chama.

“Mwenyekiti wa Chama (anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa), Profesa Ibrahim Lipumba, aliniagiza niitishe kikao hiki na nilifanya hivyo kwa kuwatumia ujumbe wajumbe wote bara na visiwani, lakini hakuna mjumbe hata mmoja wa upande wa Zanzibar aliyejibu.

“Mpaka kufikia saa 4:15 asubuhi, wajumbe wote wa bara walikuwa wameshafika makao makuu ya chama lakini hakuna mjumbe aliyefika hata mmoja wala kutoa taarifa za udhuru, hivyo hatuwezi kufanya kikao cha upande mmoja,” alisema Sakaya.

Wakati huo huo, Profesa Lipumba alisema tangu Septemba 23, mwaka jana alikuwa akitoa wito kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, ili aje ofisini kumpa maelekezo ya ujenzi wa chama bila jibu lolote.

Alisema Februari 2, mwaka huu pia alimwandikia memo ili aje kuzungumza mipango ya kuimarisha chama lakini memo hiyo ilikataliwa kupokelewa Ofisi za Zanzibar na memo ya Februari 11, mwaka huu ya kumtaka aitishe kikao cha kamati tendaji haikujibiwa.

 

“Kikao hiki kilikuwa kwa ajili ya utekelezaji wa maamuzi ya Baraza Kuu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, mwaka 2015 kufutwa, kutathmini uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani na madiwani 20 wa Tanzania bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles