Florence Sanawa, Mtwara
Shirika la lisilo la kiserikali la Door of hope to women and youth Tanzania (DHWYT), limezindua mradi wa kuwajengea uwezo wananchi na kuwasaidia kukuza ushiriki wao katika kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi, salama na nafuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema kuwa huduma za maji zinapaswa kupewa kipaumbele kutokana na umuhimu mkubwa uliopo wa huduma hiyo.
“Unajua maji ni huduma muhimu kwa kila mtu hayana mbadala kukosekana kwa huduma hiyo kunaweza kuleta athari kubwa ndani ya jamii ndio maana sehemu ambayo haina maji inakuwa na migogoro mingi kushirikishwa kwa wananchi Katika mradi wa maji unaweza kuwa msaada mkubwa,” amesema.
“Unajua maji yanasumbua sana ndio maana yanapokosekana hata migogoro kwenye ndoa inakuwa mingi hata watoto mashuleni wanakuwa watoro” amesema Mmanda.