31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa maji wazinduliwa Mtwara

Florence Sanawa, Mtwara

Shirika la lisilo la kiserikali la Door of hope to women and youth Tanzania (DHWYT), limezindua mradi wa kuwajengea uwezo wananchi na kuwasaidia kukuza ushiriki wao katika kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi, salama na nafuu. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema kuwa huduma za maji zinapaswa kupewa  kipaumbele kutokana na umuhimu mkubwa uliopo wa huduma hiyo. 

“Unajua maji ni huduma muhimu kwa kila mtu hayana mbadala kukosekana kwa huduma hiyo kunaweza kuleta athari kubwa ndani ya jamii ndio maana sehemu ambayo haina maji  inakuwa na migogoro mingi kushirikishwa kwa wananchi Katika mradi wa maji unaweza kuwa msaada mkubwa,” amesema.

“Unajua maji yanasumbua sana ndio maana yanapokosekana hata migogoro kwenye ndoa inakuwa mingi hata watoto mashuleni wanakuwa watoro” amesema Mmanda. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles