28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa maji kuwanufaisha wakazi 15,425 Shinyanga

Na Anthony Ishengoma, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Yasinta Mboneko, amezindua mradi wa maji wa Mawaza- Negezi wenye thamani ya takribani bilioni 1.5 ambao utawanufaisha wakazi wapatao 15,429 wanaoishi katika vitongoji vinane vilivyoko nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga.

Yasinta  Mboneko amezindua mradi huo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ujulikanao kama Mawaza -Negezi ulioko  nje kidogo ya  Maspaa ya Shinyanga ambao umefunguliwa katika maadhimisho ya Wiki ya Maji Mkoani Shinyanga.  

Mboneko amewataka wasimamizi wa mradi huo ambao ni Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kuhakikisha wafanyakazi wanaosimamia mauzo ya maji katika vizimba 27 vya mradi huo wasishindwe kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa visingizio vyovyote na endapo ikitokea wamepatwa na changamoto ya dharula basi awepo mbadala wa kufanya kazi hiyo.

Aidh,a Mkuu huyo wa Wilaya ya Shinyanga amezitaka Mamlaka za maji Shinyanga na Taasisi nyingine Mkoani humo kuhakikisha zinazingatia sheria katika kulinda miundombinu ya maji pamoja na mazingira kwa miradi ambayo serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha inawanufaisha wananchi kwa ajili ya maendeleo kwa manufaa ya vizazi na vizazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga, Yusuph Matopola amesema kuwa awali mradi huo ulikadiliwa kupewa mkandarasi ambaye angetumia kiasi cha Sh bili 3 lakini baada ya serikali kuanzisha mfumo wa akaunti ya dharula mradi huo mpaka kukamilika kwake utatumia takribani bilioni 1.4 na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kwani mpaka sasa (SHUWASA) ishatumia kiasi cha Sh bil 1.18 na mradi huo ushaanza kufanya kazi.

Wakati huo huo mwananzengo, Mwatano Salum, ameishukru Serikali kukamilisha mradi huo wa maji kwani wakazi wa eneo hilo kwa miaka mingi wamekuwa wakilazimika kwenda umbali mrefu kutafuta maji na wakati mwingine kukesha Kisimani wakitafuta maji au kuamka usiku wa manane kufuata maji hivyo mradi huo umekuwa mkombozi kwa jamii hiyo.

Aidha, Lukasi Kulwa mkazi wa Mawaza Shinyanga aliongeza kuwa ukiachilia mabali kero ya maji kwa kipindi cha kiangazi ndoa za wakazi wa eneo hilo zilikuwa zikiingia mashakani kutokana na wanadoa wengi kupoteza muda mwingi wakifuatilia maji na hivyo kupunguza muda wa kujenga mahusiano yao.

Mradi huu Mwawaza –Negezi umezinduliwa katika wakati Taifa likiadhimisha wiki ya maji ambayo imeanza leo na kilele cha Wiki hii kitakamilika ifikapo Machi 22, ambapo miradi mbalimbali ya maji itazinduliwa katika Halmashauri mbalimbali za mkoa wa Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles