26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Vijiji 32 havina maji safi kilimanjaro

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Vijiji 32 kati ya Vijiji 519 mkoani Kilimanjaro havijapata huduma za maji safi na salama ambapo miradi 76 inaendelea kutekelezwa na kwamba inatarajia kukamilika Juni 2021.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Moshi leo Jumanne Machi 16,2021 katika wiki ya Maji inayohusisha Mamlaka za Maji ikiwemo Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) na Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Meneja wa RUWASA Mkoa, Weransari Munisi, amesema kwa kipindi cha Mwaka mmoja wameweza kukamilisha miradi 11 na miradi 76 iliyobaki inatarajiwa kumalizika kabla ya June, 2021.

Amesema Mawakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kuzindua miradi 11 yenye thamani ya Sh bilioni 4.6 ambayo imelenga kwenye kata 17 huku miradi 27 ikiendelea thamani ya Sh bilioni 5.1.

Munis amesema katika Wiki ya Maji iliyo anza leo Machi 16 hadi 22, 2021 ambapo shughuli mabalimbali zitafanywa na Mamlaka hizo ikiwemo kufanya usafi katika Mto Rau, Kupanda miti, kutoa elimu kupita vyombo vya habari.

Amesema mpango wa RUWASA ni kuhakikisha ifikapo Mwaka 2025 Mkoa huo unafikia asilimia 95 ya huduma ya maji vijijini, na kwamba kwa mwaka wa fedha 2021/22 unaokuja wametenga Sh bilioni 9.5 kwa ajili ya kujenga miradi 30 kwenye maeneo ya vijijini.

Naye Kaimu Mkuregenzi wa (MUWSA), Kija Limbe, amesema katika swala la ulipaji wa ankara za maji, wananchi wanajitahidi kwa kiasi kikubwa kulipa bili zao kwa wakati ila changamoto kubwa ipo katika Taasisi za Umma ambazo zimekuwa hazilipi bili na kusema MUWSA inazidai Sh bilioni 2.8 taasisi hizo hali ambayo ina waathiri katika uendeshaji wa shughuli za utoaji wa maji.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuregenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Philipo Patrick, katika wiki ya Maji amesema katika wiki ya maji wataendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu utunzaji wa vyanzo pamoja usafishaji mito na upandaji wa miti kwenye vyanzo vya maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles