24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

MPANGO APINGANA NA UGUMU WA MAISHA

Na JANETH MUSHI – ARUSHA


philip-mpango1WAKATI idadi kubwa ya wananchi wakilalamikia ugumu wa maisha unaowakabili, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Arusha na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa.

“Tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

“Mbali na Repoa, zipo taasisi nyingine ambazo zinaendelea na uchambuzi wa mwenendo wa uchumi wa nchi.
“Nilishasema bungeni na narudia tena, kwamba kwa vigezo vyote vya kimataifa, tutaendelea  kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwani hata Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), limetoka hapa nchini hata mwezi haujapita, nao wamechambua mwenendo wa uchumi wetu na kusema uchumi wa nchi yetu ni mzuri.

“Maneno yanayosemwa mitaani, kwamba hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko yanaenezwa na wapiga dili.

“Katika hili, nawatoa hofu wananchi, kwamba hali ya uchumi iko imara na hayo maneno yanayosemwa si ya kweli bali tufanye kazi kwa bidii,” alisema Dk. Mpango.

Alisema pia kwamba deni la taifa na mauzo ya ndani na nje yanakwenda vizuri ingawa ukame unaonyemelea nchi, unaweza ukasababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa.

Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alizishauri benki na taasisi nyingine za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi kwa kuwashirikisha kutoa mchango wa kifedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles