24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho: Wapinzani wana furaha Chelsea kufungwa

José MourinhoLONDON, ENGLAND

BAADA ya Chelsea kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wake Everton juzi katika michuano ya Ligi Kuu England, Kocha Jose Mourinho amesema anaamini wapinzani wake wana furaha kubwa baada ya kupoteza mchezo huo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini England, wameanza vibaya michuano hiyo msimu huu baada ya kucheza michezo mitano na kuwafanya washike nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi huku wakiwa na pointi 4, hivyo Mourinho anaamini wapinzani wake wana furaha kuona anapoteza michezo yake.

“Hakuna kocha sahihi wa kuweza kuipa mataji Chelsea zaidi yangu bila ya kujali matokeo mabaya kuanzia mwanzo wa msimu huu.

“Ninajua wapinzani wangu wana furaha kubwa kuona napoteza michezo yangu, lakini ninaamini kwa matokeo haya yananifanya niwe na mipango mipya ya kuonesha ubora wangu, sina wasiwasi na hali hii kila kitu kitakuwa sawa.

“Nipo hapa kwa ajili ya kazi ninaamini ni kocha sahihi wa klabu hii hakuna ambaye anaweza kufanya kama kile ambacho ninakifanya,” alisema Mourinho.

Hata hivyo, Maourinho amesisitiza kuwa bado ana nafasi nzuri ya kuendelea kutetea ubingwa japokuwa amepoteza michezo mitatu ya mwanzo huku akishinda mchezo mmoja na kutoa sare mmoja.

“Kila kitu kinawezekana lakini inategemea na jinsi tutakavyobadilika katika michezo ijayo, hata kama tukishinda kila mchezo kuanzia sasa pia inategemea na walio nafasi za juu kufanya vibaya.

“Ninaamini kuna watu wanaamini kuwa Chelsea mwakani haiwezi kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini ukweli ni kwamba kila kitu kinawezekana,” aliongeza Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles