30 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 25, 2022

Drake: Serena hakuwa na bahati

DrakeNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki kutoka nchini Canada, Aubrey Graham ‘Drake’, amesema bingwa wa tenisi duniani, Serena Williams, hakuwa na bahati katika hatua ya nusu fainali ya mchezo wa tenisi dhidi ya Roberta Vinci.

Inasemekana kuwa Drake anatoka na mwanadada huyo ambaye ametolewa katika michuano ya wazi ya US nchini Marekani.

“Serena alionyesha uwezo wake lakini hakuwa na bahati katika mchezo huo, wengi tulikuwa na matumaini kwamba anaweza kuingia hatua ya fainali, lakini haikuwa siku yake na ndiyo maana akatolewa,” alisema Drake.

Iko wazi kuwa msanii huyo amekuwa anatokea katika michezo mbalimbali ambayo Serena anacheza hata katika fainali za Wimbledon zilizomalizika mwezi uliopita na baada ya hapo walionekana kuwa pamoja katika mazingira ya mapenzi.

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,563FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles