25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Messi afurahia mtoto kwa kuiua Atletico

MessiBARCELONA, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi, juzi alifurahia kupata mtoto wa pili wa kiume huku akiipa ushindi klabu yake dhidi ya Atletico Madrid katika michuano Ligi Kuu nchini Hispania.

Mke wa Messi, Anonella Roccuzzo, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kiume na kumpa jina la Mateo, hivyo alishindwa kufanya mazoezi ya mwisho na klabu yake kwa ajili ya kuangalia afya ya mke na mtoto wake.

Hata hivyo, katika mchezo wa juzi alitokea benchi katika dakika ya 60 na kuipa klabu yake bao la ushindi baada ya kukuta moja moja.

Messi baada ya kupachika bao hilo alionekana kuwa na furaha kubwa na kuanza kunyonya kidole huku akiashiria kuwa amepata mtoto.

Atletico walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilifungwa na Fernando Torres huku Neymar akisawazisha kwa mkwaju wa adhabu kabla ya Messi kuhitimisha bao la pili baada ya kuwatoka mabeki wa Atletico.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles