25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MOURINHO: SISHANGAI FRANK DE BOER KUFUKUZWA

MANCHESTER, ENGLAND


KOCHA wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ambaye haishiwi maneno, amedai kuwa hashangazwi na kitendo cha uongozi wa klabu ya Crystal Palace kumfukuza kocha wake, Frank de Boer.

Crystal Palace amefikia maamuzi hayo baada ya kupoteza michezo yote minne ya ligi kuu tangu kufunguliwa Agosti mwaka huu.

Baada ya kocha huyo kupoteza michezo mitatu, klabu iliweka wazi kuwa wamempa mchezo mmoja dhidi ya Burnley mwishoni mwa wiki iliyopita endapo ataupoteza basi utakuwa mwisho wa kibarua chake, hivyo De Boer akaupoteza mchezo huo na kisha kufukuzwa mapema wiki hii.

Kocha wa Man United, Mourinho amedai kufukuzwa kwa De Boer hakujamshtua kwa kuwa ni kitu cha kawaida kwa makocha duniani.

“Niliwahi kufukuzwa na Chelsea mara baada ya kuwapa ubingwa, hata hivyo aliyekuwa kocha wa Leicester City, Claudio Ranieri, alifukuzwa na klabu hiyo mara tu baada ya kuwapa ubingwa wa ligi.

“Frank de Boer amefukuzwa baada ya kupoteza michezo minne ya mwanzo katika michuano ya ligi kuu, ninaamini msimu ujao tunaweza kuona kitu kingine tofauti na hicho, hivyo siwezi kuona kushangazwa kocha huyo kufukuzwa.

“Hivyo ndivyo soka lilivyo na ndio dunia tunayoishi kwa sasa, kuna makocha watakuwa na wakati mgumu na wengine watakuwa na furaha hadi mwisho wa msimu, ni mambo ya kawaida sana.

De Boer amefukuzwa kazi ikiwa ni siku 77 tangu uongozi wa klabu hiyo umpe jukumu la kuwa kocha mkuu kwa mara ya kwanza, baada ya msimu uliopita kufukuzwa kwenye kikosi cha matajiri wa nchini Italia, Inter Milan.

Crystal Palace kwa sasa ipo kwenye mipango ya kumpa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson. Uongozi wa timu hiyo umetenga kitita cha pauni milioni 2.5 ili kumsajili kocha huyo.

Hata hivyo, mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Ian Wright ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo kwenye kituo cha utangazaji cha BT Sport, ametumia ukurasa wake wa Twitter kumpa pole De Boer.

“Ni kipindi kigumu kwa De Boer, lakini anatakiwa kukubaliana na matokoe, nadhani Crystal Palace imefanya maamuzi sahihi kwa ajili ya kuilinda timu yao, lakini nampa pole kocha huyo kwa changamoto aliyoipata,” alisema Wright.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles