28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

IBRAHIMOVIC: DUNIA ITAJUA LINI NINARUDI

MANCHESTER, ENGLAND


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, amedai hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na dunia itajua lini anaungana na kikosi chake tayari kwa kushiriki michuano.

Mchezaji huyo raia wa nchini Sweden, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la goti tangu Aprili mwaka huu, tangu hapo hadi sasa hajafanikiwa kurudi uwanjani, lakini ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo vizuri.

Hata hivyo, kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, aliweka wazi kuwa mchezaji huyo anaweza kuungana na wenzake Januari mwakani kwa ajili ya ushindani, ila mchezaji mwenyewe muda mfupi ujao dunia itajua lini anarudi uwanjani.

“Nimekuwa nikisumbuliwa na goti kwa muda mrefu, lakini napenda mashabiki wangu wawe wavumilivu, nikiwa tayari kurudi uwanjani dunia yote itajua,” alisema Ibrahimovic.

Hata hivyo, mchezaji huyo alituma video kwenye ukurasa wake wa Instagram akimwambia kocha wake Mourinho, kwamba yupo tayari na muda wowote ataungana nao.

Mchezaji huyo akirudi kikosini atakutana na ushindani wa hali ya juu dhidi ya nyota mpya wa timu hiyo, Romelu Lukaku aliyejiunga na kikosi hicho kwa kitita cha pauni milioni 75 akitokea Everton katika kipindi hiki cha kiangazi.

Ujio wa Lukaku ulikuja kwa lengo la kutaka kuziba nafasi ya Ibrahimovic baada ya kupata majeraha na mkataba wake ukiwa unamalizika, lakini baada ya muda United waliamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.

Mwishoni mwa wiki hii Manchester United watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha Everton katika michuano ya Ligi Kuu England, United wanaongoza kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 10 sawa na Man City, wakitofautiana kwa mabao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles