20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho aitolea nje timu ya Taifa Syria

Jose MourinhoDAMASCUS, SYRIA

ALIYEKUWA kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, amekataa ombi la kumtaka awe meneja wa timu ya Taifa ya Syria.

Wakala wa kocha huyo, Jorge Mendes, ameweka wazi kwamba kulikuwa na ombi kwa kocha huyo kwenda kuifundisha timu ya Syria, lakini amewashukuru kwa kumpa nafasi hiyo ila hayuko tayari.

Inadaiwa kwamba Mourinho alitumiwa ujumbe na Shirikisho la Soka nchini Syria, lakini kocha huyo amedai kwamba kwa sasa anaangalia klabu za nchini England.

“Anashukuru sana kwa kupewa mwaliko wa kuwa kocha wa Syria, lakini kwa sasa jambo hilo haliwezekani kwa kuwa anatafuta klabu ya kuitumikia nchini England,” alisema Mendes.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53, alifukuzwa kazi na Chelsea kwa mara ya pili Desemba mwaka jana, ambapo kwa sasa inadaiwa kwamba kocha huyo kuna uwezekano mkubwa wa kuitumikia klabu ya Manchester United japokuwa kocha huyo amedai bado hajamalizana na United.

Ripoti za wiki iliyopita zilisema Mourinho ameanza kutafuta nyumba eneo la Cheshire jijini Manchester baada ya wawakilishi wake kufanya mazungumzo na klabu ya Manchester United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles