28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal: United bado ni bora kwa Tottenham

Van GaalMANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya Manchester United kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Tottenham juzi kwenye Uwanja wa White Hart Lane, kocha wa timu hiyo, Van Gaal, amedai bado klabu yake ni bora dhidi ya Tottenham.

Kwa sasa Tottenham imeizidi Manchester United kwa pointi 12, huku United ikishika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 53, wakati Tottenham ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 65, lakini Van Gaal anasisitiza timu yake ni bora.

“Siku zote United ikikutana na Tottenham kunakuwa na changamoto kubwa sana kutokana na ubora wa klabu hizo.

“Samahani kwa Tottenham, ukweli ni kwamba Manchester United ni klabu kubwa dhidi ya Tottenham, japokuwa wameshinda lakini kwa ubora sisi tuko juu,” alisema Van Gaal.

Hata hivyo, kocha huyo bado anaamini kuwa ana nafasi ya kuingia ‘top four’ japokuwa anazidiwa na Manchester City kwa pointi nne ambapo City ina 57 katika msimamo wa ligi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles