22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Man City, PSG hapatoshi Ulaya leo

psg-vs-mcMANCHESTER, ENGLAND

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), inatarajia kuendelea leo kwenye viwanja viwili, Etihad na Santiago Bernabeu, huku Manchester City ikipambana na PSG, wakati huo Real Madrid ikicheza na Wolfsburg.

Hii ni michezo ya robo fainali ya pili ambapo lazima timu mbili ziweze kuyaaga mashindano hayo siku ya leo.

Man City vs PSG

Huu ni mchezo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Etihad jijini England ambapo Man City watakuwa wenyeji wa PSG, katika mchezo wa awali ambao ulipigwa jijini Paris nchini Ufaransa timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

Katika mchezo huo matarajio ya wengi yalikuwa tofauti na vile ambavyo ilitokea, wengi waliipa nafasi PSG ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani jijini Paris.

Man City kwa kumkosa kiungo wake, Yaya Toure na beki, Vincent Kompany, kuliwakatisha tamaa watu wengi katika mchezo huo wa awali.

Lakini mambo yalikuwa tofauti, Man City walionesha uwezo wake na kufanikiwa kuwavuta shati wapinzani wao na kumaliza kwa sare ya 2-2.

Katika mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kupigwa leo bado PSG wana wakati mgumu kwa kuwa waliruhusu mabao mengi ya ugenini.

Kwa maana hiyo ni kwamba, Man City wanahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya 1-1 au bila kufungana, wakati huo PSG wakihitaji ushindi.

Real Madrid vs Wolfsburg

Katika mchezo wa awali watu wengi walidai kwamba Madrid wamepata mteremko, lakini kilichotokea hakuna ambaye aliamini.

Wolfsburg waliweza kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kufanikiwa kushinda mabao 2-0, mchezo huo umewaweka pazuri sana kwa kuwa wanahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili waweze kusonga mbele.

Madrid wanahitaji ushindi kuanzia mabao 3-0 jambo ambalo linaonekana kuwa ngumu japokuwa chochote kinawezekana katika soka. Kuna uwezekano mkubwa Madrid wanaweza kuiaga michuano hiyo katika mchezo huu wa leo labda Zinedine Zidane aoneshe maajabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles