30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho ahofia Ligi ya Mabingwa msimu ujao

MourinhoLONDON, ENGLAND

KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amekiri kwamba itakuwa vigumu kwa timu yake kufuzu kwa Klabu Bingwa
barani Ulaya msimu ujao kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita klabu hiyo ilikuwa kwenye uwanja wa nyumbani Stanford Bridge na kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Bournemouth, kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini England.

Kichapo hicho ni cha nane katika michezo 15 ya Ligi Kuu, kimewaacha mabingwa hao watetezi wakiwa katika nafasi ya 14 huku wakiwa na alama 15.

“Michuano imekuwa migumu sana msimu huu, lakini lengo letu kubwa lilikuwa ni kumaliza katika nne bora,
ila hali imeonekana kuwa tofauti.

“Kabla ya mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, fikra zetu zilikuwa ni kuingia katika nafasi nne za juu, lakini kwa sasa inatupa wakati mgumu na itatufanya tufikiri kuingia sita bora, hivyo ni ndoto kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema Mourinho.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kwamba klabu hiyo haiwezi kushuka daraja kama watu wanavyodhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles