29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane amkingia kifua Benzema Ufaransa

000_119461254-1MADRID, HISPANIA

NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa na Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane, amekitaka Chama cha soka nchini humo (FFF), kulitupilia mbali suala la Karim Benzema la kashfa ya kumiliki mkanda wa ngono.

Chama hicho kwa kushirikiana na waziri wa michezo nchini humo, walisema wanaendelea na uchunguzi ili kuhakikisha kama kweli mchezaji huyo anahusika katika vitendo hivyo na kama anahusika anatakiwa kufungiwa maisha kuitumikia timu hiyo ya taifa.

Ufaransa watakuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Euro mwakani, hivyo Zidane anamkingia kifua mchezaji huyo ili aweze kutoa mchango wa kuisaidia timu hiyo katika michuano ya Euro.

“Tunatakiwa kungoja hadi Alhamisi yatakapotolewa maamuzi kutokana na uchunguzi unaoendelea, lakini kitu muhimu ni kumsaidia kuona uwezekano wa kuendelea kulitumikia taifa lake.

“Hapa tunaangalia umuhimu wa mchezaji katika taifa lake, hili ni jambo binafsi lakini kuna uwezekano wa kumsaidia ili kuona jinsi gani anaendelea kufanya vizuri katika maisha yake ya soka.

“Tunahitaji wachezaji wenye uwezo kama wake hasa katika michuano ya Kombe la Euro mwakani ambapo
tutakuwa wenyeji, hivyo ni vizuri kumuacha aendelee,” alisema Zidane.

Hata hivyo, mchezaji huyo amesema kuwa lengo lake kuwa ni kuitumikia timu yake ya taifa katika michuano
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Kombe la Euro.

“Ndoto zangu bado hazijakamilika katika kuisaidia timu yangu ya taifa, hivyo ninahitaji nafasi ili kuona uwezekano wa kutoa mchango wangu katika michuano mbalimbali,” alisema Benzema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles