26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wateketeza hosteli Chuo Kikuu Jomo Kenyatta

JKUAT-FIRENAIROBI, KENYA

MOTO usiojulikana chanzo chake umetekeza hosteli namba sita ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) mjini hapa jana, ikiwa ni wiki moja tu baada ya kukumbwa na uasi kutoka kwa wanafunzi.

Wanafunzi hao waliwavurumishia mawe maofisa wakati moto ulipoanza kuchomoza katika hosteli hiyo ya wanaume.

Moto huo ulianza jana mchana katike hosteli namba sita ya wanaume iliyopo katika kampasi kuu ya Juja ulidumu kwa saa moja kabla ya kikosi cha zima moto kuwasili kuuzima.

Wazima moto walijitahidi kuudhibiti usisambie zaidi lakini wanafunzi waliandamana wakipinga kuchelewa kuchukua hatua za kuzima moto huo.

Polisui waliitwa kutuliza hali.

Wanafunzi wa JKUAT waliendesha mgomo Jumatano wiki iliyopita wakipinga uzembe katika hospitali ya chuo, baada ya kifo cha mwanafunzi aliyechukuliwa vipimo na kituo cha afya akibainika kula chakula chenye sumu.

Ili kuzima hasira zao wanafunzi walizuia barabara ya kisasa ya Thika na kupora ghala la vyakula na maabara ya chuo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles