28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kigogo Rubada kizimbani kwa wizi

Aloyce-MasanjaNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Bonde la Rufiji (Rubada), Aloyce Masanja, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi na utakatishaji wa Sh milioni 86.

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Mshtakiwa Masanja alisomewa mashtaka manne yanayomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Waliyarwande Lema.

Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Joseph Kiula akisaidiana na Denis Lekayo, walidai mahakamani kwamba kati ya Agosti mosi hadi 10, 2010 katika Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa huyo akiwa mtumishi wa Serikali na wadhifa alionao aliiba Sh milioni 50 zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.

Katika shtaka la pili inadaiwa Masanja kati ya Novemba 10 hadi 30, 2010 aliiba Sh milioni 36 zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.

Kiula alidai katika shtaka la tatu na la nne, mshtakiwa anatuhumiwa utakatishaji wa fedha jumla ya Sh milioni 86 baada ya kujiingiza katika uhamishaji wa fedha hizo huku akifahamu kwamba fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo huku upande wa mashtaka ukidai upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 24 mwaka huu mshitakiwa huyo atakaposomewa maelezo ya awali  pamoja na kuangalia kama anaweza kupata dhamana ama la.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles