24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Benzema amjibu Waziri Mkuu Ufaransa

BenzemaPARIS, Ufaransa

MSHAMBULIAJI wa timu ya Real Madrid, Karim Benzama, ameamua kujitetea baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Manuel Valls, kukosoa uwezekano wa mchezaji huyo kuitwa na kocha wa timu ya taifa, Didier Deschamps.

Mchezaji huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba aliweza kucheza misimu 12 katika soka la kulipwa kimataifa, michezo 541 bila ya kadi nyekundu na kadi za njano 11 na kuhoji watu wanaobeza tabia yake kwenye timu ya taifa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuondolewa vizuizi juu yake na mchezaji mwenzake, Mathieu Valbuena ambao wanatarajia kurejea kwenye timu ya taifa ya Ufaransa.

Ujumbe huo kwenye Twitter  ulikuwa ukimlenga Valls ambaye hivi karibuni alisema kwamba mchezaji mkubwa wa soka ni lazima awe kioo kwa vijana ambapo baadaye aliongeza kuwa yeye si Rais wa Shirikisho la soka Ufaransa (FFF) wala kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Pia, Vills alisisitiza  kwamba suala hilo litaamuliwa na kocha ambaye anatakiwa kuwa na timu bora lakini hadhani kuna umuhimu wa Benzema kurudi kwenye timu ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles