26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mongela: Mwanza ipo kimkakati EAC

Na BENJAMIN MASESE -MWANZA


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amesema Serikali imeuweka mkoa huo kimkakati na uwekezaji kutokana na kuwa kitovu cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza mjini hapa jana, alisema ili  nchi ama mkoa wowote uweze kujulikana  kimataifa ni lazima kuwapo na matukio.

Alisema kuanzia Oktoba 25 hadi Novemba Mosi, kutakuwa na shughuli ama matukio mbalimbali yakiwamo matamasha, warsha, mikutano ya kitaifa na kimataifa ndani ya mkoa yatakayosaidia kukuza uchumi na kuibua fursa na maendeleo ndani ya jamii.

Mongela alisema kutokana na Mwanza kuwa kitovu cha EAC kutasaidia kukuza uchumi wa mkoa na jamii wakiwamo wafanyabiashara kufaidika.

“Leo (juzi) tutaanza kuadhimisha Siku ya Fimbo Nyeupe inayowahusu watu wasioona, nawaomba wana Mwanza tuungane kutatua changamoto zinazowakabili na hata kudhibiti vyanzo vinavyosababisha hali hiyo.

“Vile vile Oktoba 29-30, mwaka huu kutakuwa na kongamamo la ndege zisizo na rubani ambapo shughuli hii itakuwa ya kimataifa, kama mnavyojua teknolojia imekua, sasa ndege hizo zitakuwa zinatumwa kwenda maeneo mengine na kutoa huduma kwa jamii, mbali na matukio hayo siku zinazofuata tutakuwa na shughuli ya maadhimisho ya Siku ya Mwalimu yatakayokwenda sambamba na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kitaifa yatafanyika Mwanza,” alisema.

Pia alisema faida za kijamii na kiuchumi zitakazopatikana kwa matukio hayo ni kujenga ushirikiano ndani ya jamii, vijana kupata fursa za kuonesha vipaji vyao na wafanyabiashara wa hoteli kupata wateja.

Aliwataka wadau mbalimbali wanaohitaji uwekezaji ndani ya Mwanza kujitokeza na kupewa ushirikiano na Serikali ili lengo lao liweze kutimia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles