25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili kortini kwa kuomba rushwa ya Sh milioni moja

Na Lilian Justice -Morogoro


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro imewafikisha Ofisa Tarafa ya Kimamba, Ayubu Mvurungu na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Rudewa, Thomas Mbwilo, katika Mahakama ya Kilosa kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh milioni moja.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Janeth Machulya.

Alisema watuhumiwa hao walifunguliwa kesi ya jinai namba 365/2018 mbele ya Hakimu Timoth Lyon na kusomewa shtaka la kupokea rushwa chini ya kifungu namba 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Sarah Martin, alidai mahakamani hapo kuwa Septemba 26, mwaka huu washtakiwa hao walipokea fedha hiyo ili waandae muhtasari   utakaoonesha kwamba hati ya kimila namba 19 KLS/2238 ya umiliki wa shamba la mlalamikaji ilitolewa baada ya mkutano wa Halmashauri ya Kijiji cha Rudewa Mbuyuni kuridhia.

Washtakiwa hao walipokea fedha hizo huku wakijua wanachofanya ni kinyume na maadili yao ya kazi.

Hata hivyo, washtakiwa walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana ya Sh milioni moja na kesi hiyo itatajwa tena Novemba 9, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles