MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi, maarufu kwa jina la Mo Music, amekana tetesi kwamba anatoka na mtangazaji mmoja wa redio maarufu nchini.
“Sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari, ingawa ninafahamiana na wengi ila kikubwa huwa tunaongea kuhusu kazi, naamini muziki wangu ndiyo unaonifanya niwe maarufu, lakini siyo skendo kama hizo,” alisema Mo.
Aliongeza kwamba kutokana na kuuamini muziki wake hawezi kukubali kuchafuka kwa kashfa kwa kuwa muziki wake unajiuza wenyewe bila kuwa na kashfa za ajabu ajabu.