26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mmiliki Lucky Vincent ahukumiwa miaka minne jela

Janeth Mushi, Arusha

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imemtia hatiani Mkurugenzi wa Kampuni ya Lucky Vincent, Innocent Mushi na kumhukumu kifungo cha miaka minne na miezi sita jela au faini ya Sh milioni moja na nusu.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kumkuta na hatia katika mashtaka manne yaliyokuwa yakimkabili huku Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo Vincent Longino, aliyekuwa akikabiliwa na kosa moja, kutakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

Katika kesi hiyo watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa ya usalama barabarani iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja katika ajali iliyotokea Mei 6 mwaka 2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoa wa Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles