22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Askari, mtumishi TRA wapandishwa kizimbani

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Askari Polisi wawili na mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), waliotajwa na mfanyabiashara Ikulu kwamba wamemdai rushwa na kuzuia mzigo wake tangu mwaka 2016 wamepandishwa kizimbani.

Mfanyabiashara huyo aliwataja katika mkutano wa Rais Dk. John Magufuli na wafanyabiashara uliofanyika Juni 7, mwaka huu ikulu jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 10, kwa tuhuma za kushawishi kupewa rushwa ya Sh milioni mbili na mfanyabiashara Ramadhan Ntuzwe.

Washtakiwa ambao ni askari na namba zao ni H 4086 PC Simon Sungu, H 4810 PC Ramadhan Uwezi wa Kituo cha Polisi Osterbay na Mfanyakazi wa TRA, Charity Ngalawa.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sophia Gula aliwasomea washtakiwa shtaka linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Amedai washtakiwa wanashtakiwa kwa kushawishi rushwa, wanadaiwa Oktoba 29, 2016 maeneo ya Kimara mwisho, wakiwa wafanyakazi wa TRA na Polisi walidai rushwa ya Sh milioni mbili kutoka kwa Ntuzwe.

Washtakiwa wanadaiwa walidai rushwa hiyo kama kishawishi cha kuruhusu mzigo wake ambao unadaiwa ulikadiriwa kodi ndogo jambo ambalo lilikuwa chini ya wakubwa wao.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, Jamhuri walidai upelelezi haujakamilika na hapakuwa na pingamizi kwa washtakiwa kupata dhamana.

Mahakama ilikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano, washtakiwa walitimiza masharti wako nje kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles