23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mmiliki Steps Entertainment awaponza watumishi TRA

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), inawashikilia watumishi wanne wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mkoa wa Ilala , Dar es Salaam wanaohusika na ukaguzi na ukadiriaji wa kodi, kwa uchunguzi dhidi ya ukaguzi na ukadiriaji wa kodi walioufanya kwa bidhaa za mfanyabiashara Dilesh Solanki ambaye ni mmiliki wa kampuni ya sanaa ‘Steps Enteretainment ya jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Juni 10, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Diwan Athuman amesema watumishi hao wa TRA, wanachunguzwa kwa kosa la kutumia madaraka yao vibaya kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

“ Watuhumiwa hao wanadaiwa kutoa makadirio ya Sh. bilioni 3 na milioni mia moja kama kodi za bidhaa mbalimbali za mfanyabiashara huyo jambo linaloashiria ushawishi wa rushwa,”amesema.


Aidha Athuman amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo bado unaendelea na taarifa kamili itatolewa pale uchunguzi utakapokamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles